2 Februari 2019 - 12:55
Mmoja kati ya viongozi wa Daesh akamatwa Libya

Najeshi ya usalama nchini Libya yamefanikiwa kumkamata mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yametangazwa na shirika la habari la Reuters, ikinukuu kutoka kwa vyanzo makini vya sehemu ya tukio kuwa, vyombo vya uslama vya Libya vimefanikiwa kumkamata “Khalifah Albarq” akiwa ni mmoja miongoni mwa viongozi wakuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo ambapo alikamatwa katika mji wa Sirte, mji ambao ndio ulikuwa makao makuu ya kikundi hicho.
Kwa upande mwingine habari hizo zimetangazwa na kiongozi mmoja wa mji wa Sirte alipokuwa akithibitisha kukamatwa kwa gaidi huyo wa Daesh na kulieleza shirika la habari la Reuters kuwa kukamatwa kwa gaidi huyo kumifikiwa kufuatia mpango sekta ya usalama ya Libya bila ya kushirikiana na jeshi lolote la nje.
mwisho/290